Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wezi wavamia wapika kuku na ugali kabla ya kuiba

Tanzania Food   Ugali Na Kuku Wa Kienyeji Wa Kuchoma Wezi wavamia wapika kuku na ugali kabla ya kuiba

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji wa Kijiji cha Chamasilihi katika Kaunti ya Vihiga wamebaki vinywa wazi baada ya wezi kuvamia nyumba ya bibi mmoja kijijini hapo na kuchinja kuku wake, kisha kupika kitoweo cha kuku na ugali kabla ya kuiba.

Kwa mujibu wa taarifa za tukio hilo, wezi hao baada ya kula ugali na kuku wanadaiwa kuiba kuku wengine 14 kwa bibi huyo aliyefahamika kwa jina la Jane Mudanya, ambaye alikuwa safarini Kisumu.

"Niliingia nyumbani kwangu na na kupatwa mshangao mkubwa, niligundua kwamba kuku wangu 14 hawakuwepo. Nilipoingia jikoni nilinukiwa na mchuzi wa kuku," Mudanya alisema.

"Nilitarajia kuwauza kuku hao ili nipate faida ndipo niweze kulipia wanangu karo ya shule, ilia sikujua kwamba ningebaki na banda tupu," Mudanya alilalamika.

Mudanya amewataka maafisa wa usalama kupiga doria katika eneo hilo, ili kuwakamata wezi hao.

"Vijana wa eneo hili ni wavivu. Wanakataa kufanya kazi na kutegemea kuvuna kutokana na jasho la mtu mwingine. Wanapswa kukomeshwa," Mudanya alisema.

Bibi huyo ameitaka serikali ya kaunti kuunda nafasi za ajira kwa vijana, kama njia mojawapo ya kupunguza visa vya ukosefu wa usalama na wizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live