Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wezi wa mafuta ya SGR watiwa mbaroni

SGR Watiwa Mbaroni Wezi wa mafuta ya SGR watiwa mbaroni

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewakamata watu wanne wanaodaiwa kupokea na kuuza mali ya wizi ikiwemo mafuta ya dizeli lita 850 ambayo yanadaiwa kuibwa kwenye ujenzi wa reli ya kisasa SGR, pikipiki mbili, mapipa, madumu na mipira vilivyokuwa vinatumia kusafirishia na kuhifadhia mafuta.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amewataja watu hao kuwa ni Wilbert Costantine, Mihambo Elias, Paschal Abdalah na Steven Jacob.

Amesema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na oparesheni iliyoanza mwanzo mwa mwaka huu hasa katika maeneo inayopita reli hiyo ya kisasa, ambapo jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu hao huku wengine wakiendelea kusakwa.

‘Sasa bwana huyu tumempeta pamoja na kwamba alikuwa anajificha muda mrefu kwa kuhama hama lakini pia tarehe 4 mwezi wa pili mwaka huu katika Kijiji cha Mantare tarafa ya Ngula wilayani Kwimba tulikamatwa madumu 16 yenye mafuta ya dizeli yakiwa yamefichwa kwente shamba la mahindi la bwana mmoja anayeitwa Safari Peranya huyu bwana alikimbi bado tunamtafuta na tutamkamata na kumuwajibisha kwa kuhifadhi mali ya wizi’.

Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amesema Kijiji cha Hundya Kwimba alikamatwa mpokeaji wa mafuta Paschal Abdalah ana miaka 20 ni msukuma mkazi wa mkoa wa Shinyanga akiwa na pikipiki iliyobeba mafutaya dizeli lita 190.

Kamanda Mutafungwa amewaonya wafanyakazi wa mradi huo wasio waaminifu na kusema wakibainika hatua za kisheria zitachukuwa dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live