Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wezi mafuta ya SGR wakamatwa na pesa za Nigeria, Vietnam, China, Kuwait na Combodia

Kamanda Shyyyy Wezi mafuta ya SGR wakamatwa Shinyanga

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limekamata Lita 910 za mafuta ya dizeli yaliyokuwa yakitumika kwenye ujenzi wa reli ya kisasa SGR, katika msako wa polisi wamekamata pia mipira iliyokuwa ikitumika kufyonza mafuta hayo na kwenda kuuza kwenye migodi kwa wachimbaji.



Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema katika msako huo pia wamekamata watuhumiwa tisa wa ujambazi ambao wanadaiwa kuhusika katika tukio la kuvamia kambi ya raia wa kichina wanaojenga reli ya SGR eneo la Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni pamoja na kukamata bunduki moja kwenye kambi hiyo aina ya Shotgun pump-action.



Aidha pia walikamata fedha za nchi mbalimbali ikiwemo Naira 16,000 za Nigeria, Doĺlar 100500 za Vietnam, Yuan 20 za kichina Dinar 1.5 za Kuwait na Rial 900 za Combodia ambazo ziliporwa na majambazi na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live