Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenzake Mdee waanza kuhojiwa mahakamani

Mdee Mahakamani Wenzake.jfif Wenzake Mdee waanza kuhojiwa mahakamani

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Kesi ya wabunge wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya chama chao hicho cha zamani imeanza kuunguruma mahakamani, baada ya kukwama mara tatu.

Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, imeanza kusikilizwa leo Ijumaa Oktoba 7, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha, ambapo mawakili wa Chadema wameanza kuwahoji walalamikaji hao kuhusiana na malalamiko yao.

Hatua ya kuwahoji baadhi ya walalamikaji inatokana na maombi ya mawakili wa Chadema wanaoongozwa na Peter Kibatala ambao waliomba siku ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo wapewe nafasi ya kuwahoji walalamikaji wanane kati yao, akiwemo Mdee na wenzake saba.

Mbali na Mdee wengine walioitwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga na Cecila Pareso.

Wa kwanza kuwekwa kikaangoni leo Ijumaa ni Tendega, aliyekuwa katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), ambaye amehojiwa na Wakili Kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa Chadema.

Katika mahojiano hayo, Kibatala anamuuliza kuhusiana na madai au malalamiko yake kama alivyoyaweka katika kiapo chake, pamoja na mambo mengine akidai kufukuzwa uanachama bila kufuata utaratibu kwa kutokupewa haki ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakati Wakili Kibatala akimhoji Tendega kuhusiana na madai yake hayo, katika majibu mengine amekuwa akidai hajui huku mengine akikiri kuwa hajawasilisha mahakamani ushahidi hususani vilelezo kuthibitisha madai yake hayo.

Lakini pia amehojiwa kuhusiana na taratibu za ushughulikiaji matatizo ya wanachama wanaotuhumiwa ukiukwaji wa taratibu kanuni na katiba ya chama.

Pamoja na mambo mengine, wanalalamikia kuitwa kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu kwa njia ya WhatAsapp lakini alipopewa Katiba ya Chadema inatambua matumuzi ya tehema kama moja ya njia za mawasiliano.

Pia, amekiri hakuwahi kuandija barua kuwataka Katibu Mkuu, John Mnyika na mwenyekiti, Freeman Mbowe wasishiri kikao cha Baraza Kuu walikokata rufaa kupinga uamuzi wa kamati kuu kwa madai walioa kauli za kuwahujumu hata kabla ya vikao.

Kutokana na mahojiano hayo, shauri hilo limeahirishwa kwa saa moja kwa ajili ya maandalizi ya mahakama kuangalia vilelezo vya ‘flash disketi’ mbili kusikilizwa kauli walizozizungumza Mnyika na Mbowe ambazo wanazilalamikia.

Chanzo: mwanachidigital