Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri aliyehusishwa na ubakaji atumbuliwa

RAPE Waziri aliyehusishwa na ubakaji atumbuliwa

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemwachisha kazi waziri aliyetajwa katika uchunguzi wa ubakaji, Damien Abad katika mabadiliko ya baraza la mawaziri baada ya muungano wake tawala kupoteza wingi wa viti katika uchaguzi wa bunge.

Ikiwa tu ni mwezi mmoja na nusu baada ya mabadiliko yaliyopita, mawaziri wa mambo ya kigeni, fedha na ulinzi walibaki katika nyadhifa zao lakini Macron alifanya mabadiliko katika nyadhifa nyingine muhimu.

Mkurugenzi wa shirika la Msalaba Mwekundu la Ufaransa Jean-Christophe Combe ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mshikamano na uwiano wa kijamii baada ya tuhuma dhidi ya Damien Abad, ambaye anakanusha kufanya kosa lolote, katika kashfa ambayo imeiaibisha serikali.

Damien Abad aliyetumbuliwa.

Mchumi mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo Laurence Boone ameteuliwa kuwa waziri mpya wa masuala ya Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live