Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Nchemba aagiza Polisi kuziachia pikipiki wanazozishikilia zenye makosa madogo (+Video)

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.



Dkt. Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa yq kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatua haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi waelekezeni na waliowabishi waerekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu

Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mrundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila anapopita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogo.

Chanzo: bongo5.com