Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Masauni: Matukio ya mauaji yananikosesha usingizi

MASAUNI 1 Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, amesema tangu ateuliwe kuongoza Wizara hiyo yapo mambo mawili yanayomnyima usingizi ikiwemo mauaji yanayotekelezwa na baadhi ya watu kwenye jamii pamoja na baadhi ya askari kufanya vitendo kinyume na maadili.

Waziri Masauni amesema hayo baada ya kushuhudia onesho la medani za kivita lililoandaliwa na askari wanaotarajia kuhitimu kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika kambi ya kivita ya Kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

"Tokea nimeingia, kuna vitu viwili vikubwa sana vinanikosesha usingizi, si mimi tu nina hakika, kwanza Amiri Jeshi Mkuu na watanzania wote walio wema, la kwanza kuna matukio ya mauaji mengi toka nimekabidhiwa hii nafasi nasikia leo mtu amechinjwa ukiuliza sababu unaambiwa ni wivu wa mapenzi mwingine sijui alikuwa amedhurumiwa, la pili kumekuwepo na askari wachache ambao wanatia doa jeshi la polisi," amesema Waziri Masauni

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi nchini limejipanga kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo wa kutumia silaha za moto na kwamba hakuna mhalifu atakayefanikiwa kutekeleza tukio la kihalifu.

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, kamwe Jeshi la Polisi alitomvumilia askari yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni na taratibu za Jeshi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live