Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Lugola ambana RPC Arusha mauaji ya wanawake Mto wa Mbu

42312 LUGOLA+PIC Waziri Lugola ambana RPC Arusha mauaji ya wanawake Mto wa Mbu

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mauaji ya wanawake, katika mji wa Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha, yametikisa tena ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, kutokana na wananchi na mbunge kulitaka jeshi la polisi kukomesha mauaji hayo.

Waziri Lugola ambaye yupo katika ziara mkoani Arusha, amelazimika kumpa wiki moja Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Longinus Tibishubwamu kuhakikisha wanaotuhumiwa wanakamatwa.

Katika mji huo wa Mto wa Mmbu ambao ni maarufu kwa kilimo cha ndizi na pia ni njia ya watalii wanaokwenda hifadhi za taifa za Serengeti, Manyara na Ngorongoro, hadi sasa takriban wanawake tisa wameuawa.

Akizungumza jana jioni Jumamosi Februari 16, 2019, Waziri Lugola alisema haiwezekani Serikali ya Rais John Magufuli kukubali kuendelea mauaji katika mji huo wa Mto wa Mbu na hivyo kuwakosesha wananchi amani na utulivu.

Awali mbunge wa Monduli (CCM), Julius Kalanga alimuomba Waziri Lugola kusaidia kudhibitiwa kwa mauaji ya wanawake katika mji huo kwani sasa imekuwa ni kero kubwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz