Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Kalemani aweka ndani watumishi wa radio

Watumishipic Waziri aagiza Watumishi kuwekwa ndani

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: mwananchidigital

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mathew Kundo ameagiza watumishi watatu wa Redio Sengerema ya wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kuwekwa ndani kwa muda usiojulikana kutokana na ubadhirifu wa Sh28 milioni

Wafanyakazi hao ni ofisa habari Halmashauri ya Sengerema, Silvanus Mdalami, meneja wa kituo hicho, Sostenes Tangalo pamoja mwanasheria Ilambona Mahuba.

Amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea kituo hicho na kubaini kuwepo kwa ubadhirifu huo.

Amesema wizara ilikipatia Kituo hicho Sh103 milioni kwa ajili ya kukisaidia Kituo hicho lakini katika uhakiki walibaini Sh28 milioni hazijulikani zilipo.

Mbunge wa Sengerema (CCM), Hamisi Tabasamu amesema watumishi wa Halmashauri ya Sengerema si waadilifu kutokana na kutafuna fedha za Serikali.

Chanzo: mwananchidigital