Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili watiwa hatiani kujifanya maofisa Usalama

Hukumu Pc Data Wawili watiwa hatiani kujifanya maofisa Usalama

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Verified MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewatia hatiani na kuwahukumu kulipa faini au vifungo vya miaka miwili kila mmoja, Joshua Kamalamo na Yahya Kapalatu kwa makosa ya kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (DDPP) kama maofi sa usalama kutoka ofisi ya Rais.

Mtuhumiwa namba moja, Joshua Kamalamo amekutwa na hatia katika mashtaka mawili ya kujitambulisha kwa mkurugenzi wa mashtaka na naibu wake kama ofisa wa usalama. Katika shitaka la kwanza Joshua alihukumiwa kulipa faini ya Shilingi 1,400,000 au kifungo cha miaka mwili gerezani na kosa la pili kulipa shilingi 1,500,000 au kifungo cha miaka miwili gerezani huku vifungo vyote vikienda kwa pamoja.

Mshtakiwa huyo alilipa faini. Mshtakiwa namba mbili, Yahya Kapalatu alikutwa na hatia katika shtaka namba mbili la kujitambulisha kwa DPP kama ofisa wa usalama na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 1,000,000 au kifungo cha miaka miwili gerezani.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu mkazi mkuu Richard Kabate alisema sheria ambayo inawashitaki inasema kuwa iwapo mtu atakutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili, faini au vyote kwa pamoja

Chanzo: www.tanzaniaweb.live