Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili washikiliwa kwa mauaji

01b45baf8b8515900775f04e3afdf45a Wawili washikiliwa kwa mauaji

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili ambao ni Dutu Maige Danga (30) Mkazi wa Kijiji Cha Nkungwi na Yusuf Sita Muge Mkazi wa Kijiji Cha Santamaria kwa kuhusika na tukio la mauwaji ya Mariam Paschal (36) na mtoto wake Editha mwenye umri wa miezi 4 na kisha kuifukia miili yao katika Pori la akiba Kalilankulukulu lililopo Wilaya ya Tanganyika.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad amesema mnamo Machi 8, 2022 walipokea taarifa kutoka kwa Paschal Masheku (56) kuwa binti yake aitwaye Mariam Paschal pamoja na mtoto wake walitoweka katika mazingira yenye utata tangu mwezi Julai 2021 na haijulikani alikoenda.

"Baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo, upelelezi wa kina ulianza mara moja na ndipo Machi9, 2022 watuhumiwa wawili ambao ni Dutu Maige Danga na Yusuf Sita Muge walikamatwa kuhusiana na tukio Hilo."Alisema ACP Hamad

"Baada ya kuhojiwa wote wawili kwa pamoja walikiri kumuuwa Mariam Paschal na mtoto wake Edita Dutu na miili yao kuifukia kwenye shimo katika pori la Kalilankulukulu Wilaya ya Tanganyika."Aliongeza

Mnamo Machi 12, 2022 watuhumiwa wote wawili waliwaongoza askari Polisi kuonesha mahali walipofukia miili hiyo na baada ya kufukua yalipatikana mabaki ya miili ya marehemu hao.

"Chanzo Cha tukuio hilo ni ugomvi wa kifamilia kati ya mtuhumiwa Dutu Maige Danga na aliyekuwa mzazi mwenzake aitwaye Mariam Paschal."ACP Hamad

Upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na mara utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live