Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wakamatwa tuhuma za mauaji ya watu 19 baa

Mauaji Sauzi Wawili wakamatwa tuhuma za mauaji ya watu 19 baa

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Afrika Kusini wamesema kwamba wamewakamata watu wawili wanaohusishwa na moja ya mashambulizi mawili kwenye baa ambayo yalisababisha vifo vya watu 19, tukio hilo liliibua hisia tofauti miongoni mwa wakazi wa maeneo Jirani na maeneo ambapo tukio hilo lilitokea.

Hatua ya kukamatwa kwa watu hao imetokea kufuatia uchunguzi wa kina kuhusiana na shambulizi hilo la bunduki lililotokea Jumamosi usiku kwenye baa katika mji wa mashariki wa katika jimbo la KwaZulu Natal, ambako watu wanne waliuawa na wengine wanane kujeruhiwa wakati wanaume wawili walipowafyatulia risasi kiholela wateja waliokuwemo kwenye baa hiyo.

Watu wengine 15 wakiwemo wanawake wawili, waliuawa kwa kupigwa risasi mapema Jumapili wakati wakiburudika usiku katika kitongoji cha Soweto, karibu na Johannesburg, katika tukio tofauti.

Wizara ya polisi imeeleza katika taarifa kukamatwa kwa watu hao kama hatua ya kwanza ya kuwaweka kizuizini wale wote waliopanga na kuhusika kwenye moja ya matukio hayo ya mauaji mabaya zaidi nchini mwishoni mwa wiki iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live