Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki wakishinikiza kutaka kuwaua watuhumiwa kituo cha polisi

DCP David Misime Wawili wafariki wakishinikiza kutaka kuwaua watuhumiwa kituo cha polisi

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili akiwemo mwanafunzi wa kidato cha nne wamepoteza maisha baada ya kudaiwa kuvamia kituo cha polisi Lulembela wakitaka kuwadhuru watu waliodaiwa kuwa wezi wa watoto.

Taarifa iliyowekwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, inasema vurugu hizo zimetokea jana Jumatano Septemba 11, 2024 Saa 8:30 mchana huko Lulembelea Wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Amesema katika vurugu hizo, waliopoteza maisha ni mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na miaka 18 -20 na mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Lulembela, Theresia John (18) ambaye nyumba yao inatazamana na kituo cha polisi.

Misime amesema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambulia.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika Kituo cha Polisi Lulembela ndipo wananchi wanaokadiriwa kufika 800 walifika kituoni na kuwataka Polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amedai Misime.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live