Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki kwenye mapigano na polisi Morogoro

Mkuu Wa Wilaya Mwasa, Watu Wauana Wawili wafariki kwenye mapigano na polisi Morogoro

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kuibuka kwa vurugu Kati ya Wananchi na Polisi katika Kijiji cha Ikwambi Kata ya Mofu Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa akiongea kwa njia ya simu amesema tukio hilo limetokea Oktoba 23,2022 ambapo chanzo ni Wakulima kuwafungia ndani ya Ofisi Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Wafugaji kwa lengo la kutaka kuwachoma moto baada ya kudai Viongozi hao wameshindwa kuwasaidia mashamba yao yanapovamiwa na Wafugaji na kulisha mifugo yao.

Mwasa amesema baada ya kuwafungia Viongozi hao Polisi walifika eneo la tukio kwa lengo la kuwatoa ndipo zikaibuka vurugu Wananchi wakiwarushia mawe Askari .

Amesema hadi sasa Watu wawili Mwanaume na Mwanamke ambao majina yao hajafahamika wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa akiwemo Diwani wa Kata hiyo Greyson Mgonela, OCD na Mfugaji mmoja Jamii ya Kisukuma “Tunaendelea kufuatilia kujua idadi kamili ya majeruhi kwani majeruhi wengine walikimbia bila kupata matibabu, taarifa kamili itatolewa badaye na IGP”

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ambaye ni miongoni mwa majeruhi Greyson Mgonela amesema wakati vurugu zinatokea Wananchi walikuwa wanatumia mawe, mikuki na marungu kuwapiga Askari huku Askari wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live