Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wadakwa wakisafirisha dhahabu vipande 28

MBARONI.jpeg Wawili wadakwa wakisafirisha dhahabu vipande 28

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema Serikali iko kwenye mchakato wa kujenga kituo cha Kanda cha madini ili kudhibiti vitendo vya utoroshwaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wanaokwepa kulipa kodi.

Homera amesema hayo leo Jumapili, Novemba 12, 2023 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na kukamatwa kwa watu wawili (majina yamehifadhiwa) wakisafirisha vipande 28 vya madini ya dhahabu kilogramu 1.08373 vyenye thamani ya Sh142.2 milioni.

Amesema watuhumiwa hao wamekamtwa usiku wa kuamkia Novemba 11 mwaka huu majira ya saa 6 baada ya kikosi kazi cha madini kwa kushirikiana na maofisa madini mkoa kuwa katika oparesheni ya kukabiliana na mtandao huo.

“Ushirikiano wa kikosi kazi maofisa madini mkoa ndio umefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ,huku akibainisha watafikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya uchunguzi kukamilika ”amesema Homera.

Amesema madini hayo yalikuwa yakisafishwa kwenye gari aina ya Toyota Mark X huku ikielezwa kusafirisha kwa wanunuzi mikoa mbalimbali.

“Kufuatia tukio hilo Serikali imepata hasara Sh13.2 milioni ikiwepo mrabaha Sh 8.5 milioni , ukaguzi Sh1.4 milioni, kodi ya huduma Sh426,687 na kodi ya zuio Sh2.8 milioni,” amesema

Wakati huo huo ametaka kikosi kazi cha madini kuendelea kufanya kazi kwa weredi katika kukabiliana na matukio hayo na kuonya wafanyabishara na wachimbaji wa madini kuacha mara moja tabia hiyo kwani serikali haitawafumbia macho.

Mikakati ya Serikali

Homera amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini iko kwenye mchakato wa kujenga kituo cha madini Kanda ili kukabiliana na matukio ya utoroshwaji wa madini katika Wilaya ya kimadini ya Chunya na Mkoa wa Mbeya.

“Tunashukuru udhibiti na mikakati ya Wizara ya madini kwani kwa sasa matukio ya utoroshwaji wa madini yamepungua na mwaka huu ni tukio la pili,”amesema

Kwa upande wake, Ofisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Oscar Kilowa amesema wataendelea na kudhibiti wa utoroshwaji wa madini unaofanywa na wafanyabishara wasiokuwa waaminifu.

Amesema kuwa lengo ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wachimbaji ikiwepo uhakika wa masoko sambamba na uwazi wa uwekezaji ili watanzania waweze kunufaika.

“Watanzania wengi wanajihusisha na madini hatuoni sababu ya kurejea nyuma ambako tumetoka kukabiliana na vitendo vya usafirishaji wa madini kinyume cha utaratibu na kanuni za kisheria,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live