Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wadakwa Tanzania tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya

90538 Dawa+za+kulevya Wawili wadakwa Tanzania tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Tanzania inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin kwa nyakati tofauti Desemba 29, 2019.

Akizungumza leo Jumatano Januari Mosi 2020 jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, James Kaji amewataja watuhumiwa hao ni Abuu Kimboko ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam aliyekutwa na dawa aina ya Heroin gramu 400.

Mwingine ni Pascal Lufunga mkazi wa Bwilingu Kibaha mkoani Pwani aliyekutwa na dawa zenye uzito wa gramu 133.

Hata hivyo, amesema watuhumiwa hao ambao walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu ikiwamo hapa nchini na  nje ya Tanzania wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo kwa mwaka 2019, Kaji amesema mamlaka imefanya operesheni mbalimbali na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya bangi kilo 325 zikiwahusisha watuhumiwa wawili.

Amesema mwaka 2019 mamlaka hiyo imekamata kilo 892 za mirungi zikiwahusisha watuhumiwa tisa na kilo 34 za heroin zikiwahusisha watuhumiwa watano.

“Mwaka 2019 tuliteketeza dawa za kulevya mara mbili, ambapo Agosti ziliteketezwa kilo 1.65 za heroin na gramu 547 za Cocaine katika kiwanda cha saruji jijini Mbeya na Oktoba tuliteketeza kilo 120 za heroin na kilo 70 za cocaine,”.

Amesema udhibiti wa dawa za kulevya nchini umeendelea kuimarika kwa kipindi chote cha mwaka 2019 na kuiomba jamii kuendelea kutoa ushirikiano kufuchua wale wote wanaoendeleza biashara hiyo haramu.

“Sasa hivi kuna changamoto zinajitokeza katika udhibiti ambapo watumiaji wanatumia dawa zenye vilevi vya asili hata hivyo mamlaka inaendelea kufanya operesheni,”.

“Lakini pia wamebuni mbinu mpya ambapo kwa sasa wanasafirisha kwa mfumo wa majani makavu halafu ukiwauliza wanasema ni majani ya chai, huu ni mfumo mpya ambao tumeubaini yote ni kutokana na kuimarika kwa udhibiti,” ameongeza.

Chanzo: mwananchi.co.tz