Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni wizi wa mifugo

0efb42b63b90a5dd39251f9e990053b5 Wawili mbaroni wizi wa mifugo

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi limewakamata watuhumiwa wawili wa utoroshaji wa mifugo maeneo ya mipakani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kunatokana na operesheni kubwa ya kitaifa iliyoanzishwa hivi karibuni, inayolenga kudhibiti matukio ya wizi wa mifugo na usafirishaji wa mifugo nje ya nchi bila kufuata utaratibu.

Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa hao na linaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine.

“Kupitia operesheni hii kabambe tumewakamata watuhumiwa wawili na tayari wameunganishwa na wenzao kule Arusha ili kuendelea na taratibu za kichunguzi na hatimaye wafikishwe mahakamani,” alisema Chatanda.

Aliongeza kuwa Tanga ni moja ya mikoa yenye wafugaji wengi na aliwasihi wale wanaojihusisha na vitendo vya utoroshaji wa mifugo waache mara moja, kwa sababu mkono wa sheria hautawaacha salama.

Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alizindua operesheni maalum ya kukamata watoroshaji wa mifugo na mazao yake, ambapo aliagiza watuhumiwa 67 wa utoroshaji mifugo wakamatwe kwa kuwa wanafahamika.

Chanzo: habarileo.co.tz