Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni wakidaiwa kukutwa na kete za dawa za kulevya

Tue, 16 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na kete saba zinazodhaniwa ni dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 1.75.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 16, 2019 na kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah na kwamba watu hao wamekamatwa Julai 15, 2019 eneo la Uswahilini Kata ya Bondeni manispaa ya Moshi.

Amewataja kuwa ni Said Nyari (20) na Anord Martin (29), “Kwa sasa naona watu wa Moshi wameachana na mirungi na kugeukia dawa za kulevya za viwandani ambazo ni hatari zaidi.”

“Tunaendelea na Uchunguzi kubaini ni dawa za kulevya aina gani kama ni Cocaine au Heroine. Niwasihi wananchi watoe taarifa kuhusiana na vijana wanaojihusisha na dawa za kulevya katika maeneo yao kutokana na athari zake kwa vijana na jamii kwa ujumla,” amesema kamanda huyo.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz