Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni tuhuma za kuua, kutoweka na kichwa

HUKUMU Wawili mbaroni tuhuma za kuua, kutoweka na kichwa

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

aia wawili wa Nigeria wanaotuhumiwa kuua na kutoweka na kichwa cha mwanamke mmoja huko Kasarani, Kenya, wamekamatwa huku uchunguzi ukionyesha kuwa waliishi nchini humo kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa tovuti ya Nation, watuhumiwa hao ni William Ovie Opia, ambaye muda wake wa kuishi nchini humo umeisha, na Johnbull Asbor, ambaye hakuwa na kibali chochote cha kuishi nchini humo wakati anakamatwa.

Taarifa zinasema Asbor aliwaambia wapelelezi kwamba alipoteza vibali vya kusafiria miaka miwili iliyopita.

Watuhumiwa hao walifuatiliwa na Idara ya Uchunguzi wa Jinai (CRIB) hadi kwenye ghorofa moja huko Ndenderu, Kaunti ya Kiambu na kukamatwa Jumapili.

Konstebo Wangila kutoka ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) huko Kasarani, aliiambia mahakama ya Makadara jana Jumatatu ya Januari 22, 2024 kwamba watuhumiwa hao walikuwa wakiishi karibu na eneo ambalo kichwa cha Rita Waeni kilipatikana.

Miongoni mwa vitu vilivyopatikana katika nyumba ambayo watuhumiwa walikuwa wakiishi ni pamoja na Kisu, kitambulisho cha taifa cha Mkenya (jina linahifadhiwa), simu sita, kompyuta mpakato tatu na laini za simu 10.

"Timu ya uchunguzi inatafuta kupata rekodi za simu za laini zote na namba za simu zilizopatikana ili kubaini kama walihusika katika mauaji hayo, Wangila amesema hayo katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani.

Amesema watuhumiwa hao ni hatari kwa kuwa hawana makazi maalumu yanayojulikana.

Wangila amesema watuhumiwa hao wanazuiliwa kwa siku nane katika Kituo cha Polisi cha Kasarani ambayo ni maagizo yalitolewa na Hakimu Mkuu Mwandamizi, Agnes Mwangi wa Mahakama ya Makadara, na watakuwa mikononi mwa polisi hadi Januari 31, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live