Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa mauaji ya Ngurudoto

Pingu Law Wawili mbaroni kwa mauaji ya Ngurudoto

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili Kwa tuhuma za mauaji ya Ndembora Exaud Nanyaro aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhumiwa na watuhumiwa hao Mei 20, 2024 huko katika Kijiji cha Ngurudoto Kata ya Maji ya chai Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema marehemu alifariki dunia Mei 25,2024 katika hospitali ya KCMC wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ulibaini kuwa chanzo cha shambulio hilo lililopekea mauaji hayo ni ugomvi wa wanandugu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live