Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa kusafirisha Heroin

94417 Heroin+pic Wawili mbaroni kwa kusafirisha Heroin

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Tanzania (DCEA) inawashikilia watu wawili kwa tuhuma  za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 508.163.

Watuhumiwa hao ni Sultan Ngowi(24) na Jimmy Mlaki(24) ambao walikamatwa na dawa hizo wakiwa wamezificha kwenye gari.

Akizungumza leo Jumanne Februari 4, 2020 kaimu kamishna mkuu wa DCEA, James Kaji amesema Januari 27, 2020 maeneo ya Kibo Ubungo wakiwa na gari aina ya Sienta, maofisa wa mamlaka hiyo walifanya upekuzi na kukamata dawa za kulevya za gramu 508.168.

Amesema dawa hizo zilibainika kuwa na Heroin baada ya kupelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali.

"Pia maofisa wa mamlaka hiyo walipofanya upekuzi walikamata mzani  pamoja na nyaraka mbalimbali. Watuhumiwa wanatarajiwa kupelekwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa,” amesema Kaji.

Amesema wamewakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kuwawekea mtego maeneo ya Kibo Ubungo.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz