Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa kumbaka na kumuua mwanamke wakimvunja mifupa na shingo

Mauaji Nn.jpeg Mauaji

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia Watu wawili na kumtafuta mwingine mmoja kwa tuhuma za kumbaka kisha kumuua Elizabeth Steven Peter (41) Mkazi wa Kijiji cha Mkajamila Wilayani Masasi.

"May 06,2022 katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Masasi kuliripotiwa tukio la kukutwa mwili wa Elizabeth mtaa wa Mkunguni Kata ya Migongo baada ya uchunguzi ilibainika alibakwa kisha kuuawa kwa kuvunjwa mifupa ya shingo"

"Polisi walianza upelelezi kupitia Wataalamu wa Cyber na kumkamata Innocent Ndomba (32) ambaye alikiri kuhusika na tukio kwa kushirikiana na Mume wa Marehemu Deograthias John (32) ambaye anashikiliwa pia na Polisi.

"Watuhumiwa wameleeza kuwa chanzo cha tukio ni wivu wa kimapenzi baina ya Marehemu na Mumewe ambapo inadaiwa Marehemu alikuwa akimroga Mumewe pamoja na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wanaume wengine..."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live