Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Meno Ya Tembo Wawili mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamemekamatwa wakituhumiwa kusafirisha meno manne ya tembo yenye kilo zaidi ya 120 wilayani Handeni mkoani Tanga kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu Julai 10,2023 Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Handeni, Albert Msando amesema wamekamata meno hayo yakisafirshwa kinyume na taratibu katika msako maalum wa kuthibiti uhalifu.

Amesema katika msako huo wamekamata bunduki aina ya gobole mbili, risasi zilizotengenezwa kienyeji na pikipiki ambayo ilikuwa ikitumiwa na wahalifu hao ambao nao wamekamatwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live