Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili kortini wakidaiwa kuliibia kanisa

MAKANISA Wawili kortini wakidaiwa kuliibia kanisa

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa wawili wa Masoko wa Kampuni ya Cancel Concrete wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita likiwemo la kugushi nyaraka mbalimbali zenye thamani ya Sh49.6 milioni ili kulipa Parokia ya Mji Mpya Gongo la Mboto.

Wakili wa Serikali, Tumaini Maingu ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kwamba washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kula njama, mashtaka mawili ya kugushi, mawili tena ya kuwasilisha nyaraka za uongo na moja la wizi wa kuaminika.

Katika shtaka la kwanza inadaiwa kuwa kati ya Desemba 14, 2022 na Desemba 16, 2022 eneo la kampuni Camel Concrete Wilaya ya Ilala walikula njama kutenda kosa la wizi wa kuaminika. Also Read

Wawili wapigwa risasi katika maandamano Kenya Kimataifa 36 min ago Samia atoa pongezi mama ayekumbatia watoto Amana Kitaifa 36 min ago

Katika shtaka la pili inadaiwa Desemba 14, 2022 maeneo hayo waligushi risiti ya malipo ikionyesha imelipa Parokia ya Mji mpya Gongo la Mboto kiasi cha Sh49, 680, 000 jambo ambalo walijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Shtaka la tatu tarehe hiyo na maeneo hayo washtakiwa hao walitengeneza nyaraka za uongo ambayo ya Desemba 6, 2022 kwa Parokia ya Mji Mpya ya Gongo la Mboto yenye thamani ya Sh49, 680, 000.

Katika shtaka jingine, inadaiwa tarehe hiyo na maeneo hayo waligushi risiti ya mauzo yenye thamani ya Sh49 milioni kwenda Parokia ya Mji Mpya Gongo la Mboto.

Maingu alidai tarehe hiyo na maeneo hayo washtakiwa hao wakiwa na nia ovu walitengeneza nyaraka za uongo ambayo ni risiti yenye thamani ya Sh49 milioni kwenda Parokia ya Mji Mpya Gongo la Mboto.

Shtaka la mwisho katika tarehe hiyo na maeneo hayo washtakiwa hao waliiba Sh5.6 milioni kupitia risiti ambazo walikuwa wameambiwa na Kampuni hiyo.

Upelelezi umekamilka na wameiomba mahakama hiyo ipange tarehe ya kwa ajili ya kuwasomewa hoja za awali.

Hakimu Shaidi alisema washtakiwa hao wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Taifa na kila mmoja asaini bondi ya Sh20 milioni.

"Kati ya wadhamini hao mmoja anatakiwa awe na mali isiyohamishika au hati yenye thamani ya Sh20 milioni," alisema Shaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live