Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili jela miaka mitatu kwa kusafirisha cocaine

Cocaine Wawili jela miaka mitatu kwa kusafirisha cocaine

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu wakazi wa Gerezani jijini hapa, Habibu Ibrahim Habibu na Salum Dachi kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri kosa la kusafirisha gramu 60.2 za dawa za kulevya aina ya cocaine.

Pia mahakama hiyo imetoa amri dawa za kulevya gramu 60.2 aina ya cocaine zirejeshwe kwenye mamlaka husika ili zifanyiwe utaratibu wa kuziteketeza kwa amri ya sheria pamoja na simu za washtakiwa hao kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.

Hukumu hiyo imetolewa jana Machi 9 na Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya baada ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya hizo.

Mbuya amesema upande wa mashtaka wameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kwa kuzingatia yale waliyokubaliana katika makubaliano ya awali.

Amesema katika makubaliano hayo washtakiwa hao waliiomba mahakama hiyo iwape adhabu ndogo yenye hafifu kwa sababu wamepatikana na hatia ya jinai kwa mara yao ya kwanza.

"Katika makubaliano yao wamekiri makosa yao na wamekuwa gerezani kama mahabusu tangu Desemba 21, 2020 hadi leo hii," amesema Mbuya.

Mbuya alisema kwa upande wa mshtakiwa Habibu aliiomba mahakama hiyo yeye ni yatima akiwa kidato cha tano alishindwa kulipa ada ya shule akalazimika kujiingiza kwenye dawa za kulevya ili apate ada.

Alisema kwa upande wa mshtakiwa Dachi alieleza mahakama hiyo kuwa ana familia ya watoto wanne ambao wanakaa kwa shangazi yao ambaye hana uwezo na pia ni mgonjwa

Hivyo mahakama hiyo imeangaliwa madai hayo yana mashiko hivyo washtakiwa hao wanaweza kupunguziwa adhabu kutokana na kukaa gerezani kwa muda mrefu na kukiri kosa lao inaonyesha wamejutia.

Amesema washtakiwa walikaa na upande wa Jamuhuri walikubaliana wakiri kosa lao ili waende jela miaka mitano hivyo mahakama hiyo haifungwi na makubaliano ya adhabu hiyo hivyo inaweza ikaongeza au kupunguza.

Kutokana na hilo mahakama hiyo inawahukumu kila mshtakiwa aende kifungo cha miaka mitatu jela.

Idaiwa kuwa kati ya Desemba 21, 2020 maeneo ya bandari ya Dar es Salaam washtakiwa walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya gramu 60.2 aina ya cocaine kupelekea Zanzibar.

Chanzo: mwanachidigital