Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili jela miaka 30 kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Wawili Jela Miaka 30 Kwa Kosa La Unyang'anyi Wa Kutumia Silaha.png Wawili jela miaka 30 kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yahya Matabora (38) Mkulima na Mkazi wa Majengo na Jumanne Alute (24) Mkazi wa Utemini Manispaa ya Singida wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa kosa la unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Washtakiwa walitenda kosa hilo Aprili 11, 2023 maeneo ya Barabara ya Dodoma, Kata ya Kindai, Wilaya na Mkoa wa Singida ambapo walimnyang'anya mwanamke mmoja pesa taslimu Tsh. 600,000/= kwa kutumia silaha aina ya panga.

Washtakiwa walikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa Mahakamani Juni 7, 2023 ambapo hukumu imetolewa Julai 29, 2024 na Mhe. Lucy Migani ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Singida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live