Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili jela miaka 20 kwa wizi wa ng’ombe 10

52377 Pic+jela

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara imewahukumu kifungo cha miaka 20 wakazi wawili baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya wizi wa ng'ombe 10.

Katika kesi ya jinai namba 32/2017 waliohukumiwa ni Nyigana Maro (28) mkazi wa kijiji cha Majimoto na Chacha Maro (46) mkazi wa kijiji cha Majimoto.

Akitoa hukumu leo Jumatatu Aprili 15, 2019 hakimu Jakobo Ndila amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakama yake inawahukumu kila mmoja kifungo cha miaka 20 na wote wanatakiwa kulipa faini ya Sh5.4 mil.

Mapema mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Paskael Nkenyenge amesema washitakiwa waliiba ng'ombe 10 wenye thamani ya Sh6 milioni mali ya Wambura Wambura mkazi wa kijiji cha Majimoto.



Chanzo: mwananchi.co.tz