Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili Mbaroni Kwa Tuhuma za Mauaji Mbozi

Kamanda Songwe Wawili Mbaroni Kwa Tuhuma za Mauaji Mbozi

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata kwa mapanga mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jancken Kabuje (45) mkazi wa Kitongoji cha Mantengu Kata ya Vwawa wilayani Mbozi.

Kamanda wa polisi mkoani Songwe, ACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea Disemba 26, 2021 majira ya saa tatu usiku ambapo marehemu alikuwa anarudi nyumbani kwake akitokea kazini ndipo watuhumiwa hao wakamvizia na kumkata kwa mapanga.

Kamanda Magomi amesema jeshi la polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi kubaini kuhusu tukio hilo la mauaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live