Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavunja rekodi kukamatwa na tani 32 za bangi

Bangiii Wavunja rekodi kukamatwa na tani 32 za bangi

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Hispania limesema wamekamata kiwango kikubwa cha bangi kuwahi kutokea sio tu nchini Uhispania bali kote ulimwenguni, kiasi cha zaidi ya tani 32.

Katika taarifa iliyotolewa Polisi imesema wamepata tani hizo za bangi katika miji ya Toledo, Ciudad Real, Valencia na Asturias.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, waligundua mtandao wa biashara ya bangi unaoisafirisha kote Uhispania pamoja na nchi nyingine za Ulaya zikiwamo Uswisi, Uholanzi, Ujerumani na Ubelgiji.

Katika tukio hilo, watu 20 wakiwemo wanaume tisa na wanawake 11 wa umri kati ya 20 na 59 walikamatwa na kuwekwa mbaroni kama sehemu ya operesheni ya Jeshi hilo la polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live