Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watupwa miaka 70 kwa wizi wa mifugo

Jela Miaka 30 Wahukumiwa miaka 70 kwa wizi wa mifugo

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: eatv.tv

Watu sita ambao ni majambazi sugu wa mifugo wamehukumiwa kifungo cha miaka 70 jela kwa  kosa la unyanganyi wa kutumia silaha aina ya bunduki na mapanga katika mahakama ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Hakimu Yohana Myombo ambapo washitakiwa hao  walikuwa wanakabiliwa  na mashitaka matatu  tofauti mahakamani hapo.

Hakimu Mkazi mwandamizi Miyombo amesema kuwa mahakama hiyo imethibitisha ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasi kuacha shaka lolote dhidi ya washitakiwa hao sita na kuwa tia hatiani kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu cha sheria ya makosa ya jinai no 287 A sheria ya Adhabu kilichofanyiwa mapitio mwaka 2009 na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 Katika kesi mbili na katika kesi no 238  washitakiwa hao walihukumiwa miaka 10 jela.

Awali akisoma hati za mashitaka mbele ya Hakimu Myombo  Mwendesha mashitaka wa Serikali Esther Komba amesema washitakiwa hao walikuwa 9 ambapo washitakiwa watatu waliachiwa huru kutokana na ushahidi kutowatia hatiani katika kesi hizo.   Komba ameiambia mahakama hiyo kuwa katika kesi ya kwanza no.238 ya mwaka 2021 ulikuwa linawakabili watuhumiwa saba ambao ni Boniphace Mao, Ng'ong'ona Mwita, Onyango Mwita, Peter Range, Danny Nyamongo na George Omolo Kamkono na katika kesi no.239 ya mwaka 2021 iliwakabili tena washitakiwa hao pamoja na Manko Mchuma Jobe. 

Mwendesha mashitaka Komba amesema katika shitaka no.259 la mwaka 2021 linawakabili washitakiwa watano ambapo kati ya hao washitakiwa watano watatu kati yao wanahusika katika mashitaka mawili ya mwanzo na kuwataja washitakiwa hao kuwa ni Lucas Masero,Marwa Ghati ( Marwa mkulima),Peter Range, Onyango Mwita na Ng'ong'ona Mangure.

Aidha Mwendesha mashitaka aliwataja washitakiwa walio achiwa huru na mahakama hiyo kuwa ni Danny Laban Nyamongo, George Omolo Kamkono na Manko Mchuma Jobe baada ya ushahidi kushindwa kuwatia hatiani washitakiwa hao kwa kosa la kufanya unyanganyi wa kutumia silaha.

Aidha akitolea ufafanuzi hukumu hiyo Mkuu wa Mashitaka kutoka Ofisi ya Mashitaka Wilayani Tarime Mafuru Moses anaeleza.

Baada ya Hakimu Yohana Myombo kutoa hukumu hiyo washitakiwa hao walianza kufanya fujo mahakamani hapo wakipinga hukumu waliyo pewa.

Chanzo: eatv.tv