Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watupwa jela miaka 30 kwa unyang'anyi wa kutumia silaha

HUKUMU Watupwa jela miaka 30 kwa unyang'anyi wa kutumia silaha

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imewahukumu Watu watatu kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 kwa makosa manne ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Samuel Maweda ambapo amewataja Washtakiwa hao kuwa ni Emanuel Matulanya (20), Musa Soro(20) na Philipo Lucas (18) waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka manne ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Winfrida Ernest ni Wakili wa Serikali amedai kuwa Washtakiwa hao kwa pamoja waliiba mali mbalimbali ikiwemo fedha taslimu,simu za mkononi na Laptop pamoja na kujeruhi kwa kutumia panga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live