Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi wanne Halmashauri Mbarali washitakiwa ubadhirifu TSZ milioni 11

Hukumu Pc Data Watumishi wanne Halmashauri Mbarali washitakiwa ubadhirifu TSZ milioni 11

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mnamo tarehe 29/09/2022, Mahakama ya Wilaya Mbarali ilitoa hukumu katika shauri la Uhujumu Uchumi Na. 17/2022 dhidi ya George Kagomba, Ferdinand Manyele, Ponsiano Ngwando na Yasini Kabelege.

Ambapo washitakiwa wa 1-3 Walikuwa watumishi Halmashauri ya Wilaya Mbarali kwenye nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji, Mweka Hazina na Afisa Mtendaji wa Kata mtawalia na mshitakiwa wa 4 alikuwa Makamu Mwenyekiti - Kamati ya Ujenzi katika Shule ya Sekondari Rujewa.

Washitakiwa hao walishitakiwa kwa makosa 4 ya Ubadhilifu wa shs 11,765,000/=, Kughushi, Kutumia Nyaraka kwa Lengo la Kumdanfanya Mwajiri na Kuwasilisha Nyaraka za Uongo. Mahakama kwenye uamuzi wake imewatia hatiani Washtakiwa wote 4 kwa Makosa hayo na kila mmoja kuadhibiwa kulipa fine au kwenda Jela miezi 6. Pia wameamriwa.

kurejesha kiasi chote cha shs. 11,765,000/= walichofuja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live