Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi wa benki kortini tuhuma za wizi

Law Firms In Sharjah Cover 21 02 1140x625 Watumishi wa benki kortini tuhuma za wizi

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watuhumiwa saba, wakiwamo wa Benki ya NMB wilayani Igunga mkoani Tabora, wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kughushi na kuiba zaidi ya Sh. milioni 60.

Watu hao walisomewa mashtaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora,  Gabriel Ngaije.

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ambayo wanadaiwa kuyatenda kwenye benki hiyo wilayani Igunga.

Wakili wa Serikali, Robert Kumwembe, alidai mahakamani huko kuwa watuhumiwa walitenda makosa matatu ambayo ni kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kughushi risiti za kuonyesha fedha zinazoingizwa kwenye akaunti ya mteja wao, Kija Dotto ni halali.

Watumishi wa Benki ya NMB waliofikishwa mahakamani ni Ngolo Lunengu, Ally Saidi, Prisca Shula, Sedalia Venance, Anastazia Richard, Boniface Henry na Anastazia Felix.

Kumwembe alidai watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi ya jinai ambayo waliitenda mwaka 2022 kwenye Benki ya NMB wilayani Igunga mkoani Tabora.

Watuhumiwa hao walipewa dhamana na kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 13, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live