Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi wa Tanesco wasomewa makosa 125

Hukumu Pc Data Watumishi wa Tanesco wasomewa makosa 125

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAFANYAKAZI wawili wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mwanza wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mkoa wa Mwanza wakituhumiwa makosa 125 yaliyogawanyika katika makundi matatu na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.1. - Waliopandishwa kizimbani jana wakishitakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi Na. 5 ya mwaka 2023 katika mahakama hiyo ni fundi mchundo, Abdulkadri Hussein na Ofisa Bohari, Respicius Rumanyika ambao ni wafanyakazi wa Bohari ya Tanesco- Nyakato jijini Mwanza. - Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa serikali kwa niaba ya Jamhuri Magreth Mwaseba akishirikiana na Mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, Maximillian Kyanabo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo 125 kati ya mwezi Novemba 2021 hadi Desemba, 2022 kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 ya Mwaka 2022 kuwa ni kushiriki kwenye wizi wa miundombinu hiyo ya Tanesco na kuiuza na hivyo kuisababishia serikali hasara mabilioni ya fedha. - Kwa upande wake, Mwanasheria wa Takukuru Kyanabo alidai mahakamani hapo kuwa makosa hayo yamegawanyika katika makundi matatu ambayo ni pamoja na kuongoza genge la uhalifu, kuisababishia serikali hasara na makosa ya kughushi nyaraka wakitenda makosa hayo kwa kuihujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mwanza. - Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Stellah Kiama alisema kesi hiyo imeahirishwa kwa madai kuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kisheria wa kuendesha shauri hilo na watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote na walirudishwa mahabusu hadi Agosti 10, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live