Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi mahakama kitanzini tena

19d1e26969a06086e49e69aa711d0760.jpeg Watumishi mahakama kitanzini tena

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka watumishi wa mahakama nchini kuwa na desturi ya kufanya tathmini ya huduma wanazotoa kwa jamii ili kujua kama zinakidhi matarajio ya wananchi ya upatakanaji wa huduma ya haki kwa wakati.

Akizungumza juzi jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama awamu ya pili, Profesa Gabriel alisema kuwa kwa kufanya hivyo utekelezaji wa mpango mkakati na mradi wa uboreshaji wa huduma za mahakama utafanikiwa.

“Moja ya mambo muhimu ya kuzingatia katika utekelezaji wa mpango mkakati ni kujua au kujiuliza wewe kama mtumishi ni nini unachokitoa katika jamii. Je, unatoa huduma kwa uwazi, je, huduma unayotoa inafikika kwa wananchi na je, haki unayotoa ni ya kiwango gani? Hivyo ni muhimu kuzingatia haya ili kazi iweze kufanyika kwa ufasaha,” alisema.

Aidha, Profesa Gabriel pia alitoa rai kwa watumishi kuacha tabia ya kulaumiana wakati wa utekelezaji wa majukumu badala yake wafanye kazi kama timu moja na hatimaye kutoa mrejesho wa masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za mahakama.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Wilbert Chuma aliwataka wamiliki wa maeneo ya utekelezaji wa shughuli za mradi kuwa na umiliki wa dhati wa maeneo yao. Pia aliwataka kutoa ushirikiano kwa Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama (JDU) ambacho kinaratibu utekelezaji wa shughuli zote za mradi.

Mpango Mkakati wa Pili wa Mahakama (2020-2025) utatekelezwa kwa kiasi kikubwa na nyongeza ya mkopo wa Benki ya Dunia wa dola za Marekani milioni 90 baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi uliotumia dola za Marekani milioni 65.

Kikao kazi hicho kilichohusisha washiriki 250 wakiwemo majaji, wasajili wa mahakama, watendaji wa mahakama na baadhi ya watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo wa wasaidizi wa ofisi, katibu muhtasi, watunza kumbukumbu na wengineo kililenga kufanya tathmini ya mafanikio, changamoto ya mradi wa awamu ya kwanza pamoja na mapitio ya awamu ya pili ya mradi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live