Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi Wizara ya Kilimo wafikishwa mahakamani kwa madai ya kupokea rushwa

74890 Kilimo+pc

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imewafikisha katika mahakama ya wilaya ya Ilala wafanyakazi wawili wa Wizara ya Kilimo, Flora Martin (49) na Prisca Joseph (33) kwa kupokea rushwa ya Sh100,000.

Akiwasomea shtaka hilo leo Jumatatu Septemba 9, 2019 wakili wa taasisi hiyo, Sophia Gura amedai kuwa kati ya Januari Mosi na Agosti 31, 2019 washtakiwa hao wakiwa waajiliwa wa Wizara ya Kilimo kama wakaguzi wa mazao bandarini walipokea rushwa hiyo.

Mbele ya hakimu mkazi, Flora Mjaya amesema  washtakiwa hao walipokea kiasi hicho cha fedha  kutoka kwa Tonny Joseph kama kishawishi cha kuwawezesha kumsaidia kuiruhusu mizigo yake bila kikwazo chochote.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao ambao wanatetewa na wakili , Mkama Kalebu walikana na upande wa mashtaka amedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Akitoa masharti ya dhamana,katika kesi hiyo ya jinai namba 607/2019, Mjaya amemtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh500,000.

Mshtakiwa Prisca alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru huku mwenzake akipelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo.

Pia Soma

Advertisement
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19, 2019 itakapotajwa tena.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz