Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi Tarura waomba rushwa, wadakwa na Takukuru

14939 RUSWA+PIC TanzaniaWeb

Sat, 1 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga.Watumishi watatu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) mkoani Shinyanga wanashikiliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kupokea rushwa.

Walipewa fedha hizo na wakandarasi, kwa ajili ya kuwapitisha kwenye zabuni za ujenzi wa barabara mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 31, 2018 Kamanda wa Takukuru mkoani Shinyanga, Gasto Mkono amesema baada ya kupata taarifa juu ya kuwepo kwa vitendo vya  rushwa, walianz akufuatilia na kuwakamata watumishi hao hao wakiwa na fedha hizo.

Amesema kwa sasa watumishi hao wamewekwa rumande ili kuendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Amewataja watumishi hao watatu kuwa ni Njama Kinyemi, Rose Mpuya ambao ni maofisa ugavi Tarura mkoani humo na Matoke Chiyando ambaye ni mhandisi Tarura halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

“Kwa kweli tumewakata watumishi hao watatu wa Tarura ambao walikuwa kwenye kamati ya kujadili zabuni za ujenzi wa barabara za wilaya zote mkoani Shinyanga,” amesema.

“Walikuwa wakiomba rushwa kutoka kwa wakandarasi (wamehifadhiwa) na baadhi ya fedha wameshawekewa kwenye akaunti zao, na zingine zilikuwa kwenye mabegi na mifuko.”

Amesema, “wote watatu  tunawashikilia na tunaendelea na uchunguzi zaidi, upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka yao.”

MCL Digital lilipomtafuta  mratibu wa Tarura mkoani Shinyanga,  Ezekiel Kunyarara amesema yupo safarini na na kutaka atafutwe ofisa utumishi, Jafari Mwenda ili atoe maelezo.

Mwenda amekiri kukamatwa kwa watumishi hao, kubainisha kuwa jambo hilo hawezi kulizungumza kwa kina.

 

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz