Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi Tanesco kizimbani kwa rushwa ya Sh mil 387

14fb8c4ad194713ef8870ce22d11162b.jpeg Watumishi Tanesco kizimbani kwa rushwa ya Sh mil 387

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATUMISHI watano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha kujibu mashitaka ya rushwa na uhujumu uchumi yaliyosababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 387.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, James Ruge, jana aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Maria Mwakabage aliyekuwa Ofisa Ugavi na Usafirishaji Mwandamizi na Zipporah Ngadada aliyekuwa mtunza stoo.

Washitakiwa wengine Ruge alisema ni Ruthh Dedu aliyekuwa mtunza stoo, Florencia Nyambari aliyekuwa mtunza stoo msaidizi na Michael Gumbo aliyekuwa mtunza stoo msaidizi.

Kamanda Ruge alisema uchunguzi umebaini kuwa, washitaiwa haokati ya mwaka 2016 hadi mwaka 2019 wakiwa ni watumishi wa Tanesco mkoani Arusha, walisababisha upotevu wa mali ya shirika hilo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 387.

Alisema washitakiwa hao katika kipindi hicho walibainika kuingiza taarifa za uongo katika mfumo wa kutunza kumbukumbu za bohari ili kuficha ukweli wa mali iliyopotea.

Kwa mujibu wa Ruge, washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara.

Alisema shitaka la pili ni la kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2007.

Alitaja shitaka la tatu kuwa ni watumishi hao wa umma walishiriki kuihujumu serikali kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu huku wakifahamu kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Chanzo: www.habarileo.co.tz