Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi Chato mbaroni, watuhumiwa kuiba dawa

46458 Pic+chato

Wed, 13 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chato. Watumishi watatu wa idara ya afya wilayani Chato mkoani Geita wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa dawa za aina mbalimbali zinazodaiwa kuwa ni mali ya Serikali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Machi 12, 2019 amesema kati ya watumishi wapo waganga wafawidhi wawili pamoja na mtunza stoo.

Kamanda Mwabulambo alisema watumishi hao wamekamatwa kufuatia operesheni iliyofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo na kupata taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa watumishi hao.

Alitaja dawa zilizokamatwa kuwa ni dawa za malaria aina ya Alu pakti 1080, mipira ya kuvaa mkononi box 10 zinazokaa 50 kwenye kila pakiti.

Pia watumishi hao wamekamatwa na vipimo vya malaria box 36, dawa za uzazi wa mpango 41, Alu za watoto paketi 2,292 pamoja na vipimo vya wingi wa damu.

Mkuu wa wilaya ya Chato, Msafiri Mtemi alisema kwamba  kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kukosa dawa vituoni lakini waganga wafawidhi wamekuwa wakidai dawa zipo na ndipo kamati ya ulinzi iliamua kufanya uchunguzi na kubaini wizi huo.

Alisema malalamiko ya wananchi kukosa dawa vituoni licha ya serikali kutoa dawa za kutosha yanatokana na watumishi wa afya wasio waaminifu wanaochukua dawa hizo kwa maslahi yao binafsi.



Chanzo: mwananchi.co.tz