Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi 60 mikononi mwa TAKUKURU

Mbaroni?fit=1000%2C563&ssl=1 Watumishi 60 mikononi mwa TAKUKURU

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.732 imebainika kuwa na kasoro mbalimbali katika utekelezaji wake mkoani Mtwara.

Miradi hiyo imebainika kuwa na kasoro za kutokupimwa ubora wa vifaa, kujengwa nje ya muda uliopangwa, ucheleweshwaji pamoja na kutumia vifaa chini ya kiwango

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Enock Ngailo, amesema watuhumiwa 60 wakiwemo wajumbe wa kamati wanahojiwa na taasisi hiyo na kwamba upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.

Ngailo amesema Mkoa wa Mtwara una miradi mingi ya maendeleo na kwamba hiyo ni kazi endelevu , na hivyo kuwataka wanakamati waliochaguliwa kutimiza jukumu lao la kusimamia kwa weledi miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live