Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa zaidi ya 130 wanaswa Geita

Watuhumiwa Zaidi Ya 130 Wanaswa Geita .png Watuhumiwa zaidi ya 130 wanaswa Geita

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Jeshi la Polisi mkoa wa Geita limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa zaidi ya 130 wa makosa mbalimbali ya kihalifu, ikiwemo mauaji, wizi wa silaha, mali za wizi pamoja na wahamiaji haramu

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo amesema watu hao wamekamatwa  katika operesheni mbalimbali wakifanya mkoani humo

"Tumekamata wahamiaji haramu 48, lakini pia tumekamata watuhumiwa wanaojihusisha na kuiba mazao ya misitu wanaingia kwenye hifadhi zetu 15, lakini pia tumekamata wezi wa silaha, kwahiyo jumla tumekamata watuhumiwa watatu kuhusiana na tuhuma hizo, tumekamata wavunjaji awali tuliwakamata saba walikiri na wakaweza kutajana na operesheni hii inaendelea kwahiyo mpaka sasa hivi  tuna watuhumiwa 15 wa makosa ya uvunjaji", alisema Jongo. Aidha Jongo anaelezea vifaa vilivyokamatwa kutoka kwa wahalifu hao.

"TV saba aina ya star x, tumekamata Bangi gunia saba, jumla ya pikipiki saba zenye thamani ya shilingi milioni 16 zimekamatwa lakini pia Baiskeli tisa, Redio sub woofer sita lakini pia Ving'amuzi, simu, nguo vyote hivyo ni kati ya mafanikio ya operesheni na misako tuliyoifanya lakini pia jumla ya Ng'ombe wiokamatwa ni 21 wenye thamani ya milioni 20", alisema Jongo.

Kamanda Jongo amewataka wananchi mkoani humo kuacha tabia ya kuwaficha wahalifu badala yake wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria watoe taarifa kwenye Jeshi la Polisi.

"Tunawajua wahalifu ni ndugu zetu lakini tunawaficha, tukishirikiana na Jeshi la Polisi Geita bila uhalifu inawezekana", alisema Jongo.   

Chanzo: Eatv