Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa wawili wa mauaji waachiwa huru

Waachiwa Huru (600 X 410) Watuhumiwa wawili wa mauaji waachiwa huru

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru watu wawili waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la kumuua kwa kukusudia Issa Juma, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha shitaka dhidi yao.

Washitakiwa hao Maulid Idd na Abuu Vunja wakazi wa Tandika Kilimahewa, wameachiwa huru leo mahakamani hapo na Hakimu Ramadhani Rugemalila, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya hukumu.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rugemalil, alisema wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo upande wa mashitaka walipeleka mashahidi wanne na vielelezo vitatu, ambavyo vimeshindwa kuthibitisha shitaka dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live