Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa watatu wakamatwa kwa tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 14

Thu, 1 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Jeshi la polisi la jimbo la Plateau wamewakamata wanaume watatu wanaotuhimiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 14 huko jijini Angwan Rogo nchini Nigeria.



Watuhumiwa walitambuliwa kama Suleiman Usman mwenye umri wa miaka 18, Umar Aliyu mwenye umri wa miaka 18 na Usman Bala mwenye umri wa miaka 20. Wanasemekana kuwa walimnywesha madawa mtoto huyo kabla ya kumfanyia kitendo hicho mchana wa Januari 23 mwaka huu.

Mshtakiwa mwingine anaitwa Kenza ambaye chumba chake ndicho kilicho tumika katika tukio hilo la kumbaka msichana huyo kwa sasa bado hajakamatwa na wale watuhumiwa watatu waliokamatwa wamekiri kufanya tukio hilo.

Kamishna wa PolisiUndie Adie alisema kwamba “Wanaume hao walimnywesha madawa msichana huyo ndani ya nyumba na alipo tokwa na fahamu ndipo alipo fanyiwa kitendo hicho.

Na Raheem Rajuu

Chanzo: bongo5.com