Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa wa mauaji ya watoto Njombe wafikishwa mahakamani

41379 Njombepic Watuhumiwa wa mauaji ya watoto Njombe wafikishwa mahakamani

Wed, 13 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Njombe. Watuhumiwa watatu wa utekaji na mauaji ya watoto wilayani Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakim Hakimu mkazi Njombe leo Jumanne Februari 12, 2019.

Leo ni mara ya kwanza wa watuhumiwa wa mauaji hayo yaliyotikisa mkoani Njombe kuanzia Novemba 2018 kufikishwa mahakamani.

Watuhumiwa hao ni Joel Nziku, NassonĀ  Kaduma, Alphonce Danda.

Nje ya mahakama hiyo ulinzi umeimarishwa kutokana na polisi kusambaa kila kona, huku msafara wa watuhumiwa hao ukisindikizwa na magari sita ya polisi.

Soma Zaidi: VIDEO: Mabeyo atua Njombe, atoa neno mauaji ya watoto

Soma Zaidi:Mtoto aliyekatwa koromeo wilayani Njombe afariki dunia

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz