Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa wa mauaji wapinga maelezo kuwa wanapewa chakula gerezani

94882 Pic+watuhumiwa Watuhumiwa wa mauaji wapinga maelezo kuwa wanapewa chakula gerezani

Sun, 9 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji ya mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya tembo, Wayne Lotter umeeleza jinsi ulivyofuatilia madai ya washtakiwa katika gereza la Keko na kubaini kuwa hawanyimwi chakula kama walivyodai.

Baada ya maelezo hayo, washtakiwa hao Nduimano Zebadayo na Habonimana Nyandwi

ambao ni raia wa Burundi wamesema maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka si ya kweli huku wakieleza jinsi walivyojibiwa kuwa malalamiko yao hayatafanyiwa kazi.

Januari 17, 2020 waliangua kilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakidai kunyanyaswa kutokana na uraia wao, kunyimwa chakula kwa siku tano.

Kutokana na malalamiko hayo, mahakama hiyo iliiagiza ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) kwenda katika gereza hilo kufuatilia madai hayo.

Akizungumza mahakamani hapo leo Ijumaa Februari 7, 2020 wakili wa Serikali, Faraji Nguka amedai mbele ya Hakimu mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa walipofuatilia walipewa utaratibu wa kisheria na kubaini kuwa  utaratibu wa chakula maalum kwa wafungwa watapewa ikiwa kuna taarifa za kitabibu.

Pia Soma

Advertisement
Nguka amedai wamefuatilia na hakuna mtu anayebaguliwa kwenye chakuka kwani wote wanapewa chakula sawa na mtuhumiwa anapokuwa gerezani lazima kuna haki wanazipoteza.

"Unapokuwa gerezani unapoteza haki ya kula chakula kizuri unachokitaka,  utakosa kutokana na uchumi wa nchi yetu na raia wanapokuwa kwenye magereza yetu  hayabagui mtu kutokana na utaifa wake, watu wote hupata haki sawa," amedai Nguka.

Nguka amedai mshtakiwa anapokuwa na malalamiko anatakiwa kufikisha kwa maandishi ili abaki na nakala yake, endapo suala lake halijafanyiwa kazi anaweza kwenda kwa kamishna wa Jeshi la Magereza akiwa na hiyo nyaraka aliyokuwa nayo.

Baada ya maelezo hayo, Zebedayo alinyoosha mkono na kuieleza Mahakama hiyo kuwa maelezo aliyotoa wakili huyo wa Serikali hayana ukweli.

Amesema huduma hiyo ya chakula amepewa kwa miaka miwili na hata waliotangulia wamekuwa wakipata huduma hiyo na hadi sasa raia wa kigeni wanaendelea kupata kifungua kinywa, chakula cha mchana na usiku wanapewa chai na mikate.

"Yeye anaposema huduma kama kifungua kinywa, chakula cha mchana na cha usiku ni kwa ajili ya kupewa washtakiwa ambao wametolewa taarifa ya kitabibu jambo ambalo si kweli mbona raia wa Ethiopia, Afrika kusini na Wanaigeria wanaendelea kupewa chakula hicho maalumu kwa nini sisi raia wa Burundi wasitishe, hakuna haki inayotendeka," amedai  mshtakiwa huyo.

Zebadayo amedai baada ya kutoa malalamiko hayo mahakamani hapo, walitembelewa na ofisa wa makao makuu ya gereza, aliwaeleza kuwa wataendelea kupiga kelele lakini wanayoyataka hayatafanyiwa kazi.

Hakimu Isaya baada ya kusikiliza maelezo hayo amesema hoja hizo atazizungumzia shauri hilo litakapotajwa tena mahakamani hapo Februari 21, 2020.

Chanzo: mwananchi.co.tz