Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa mauaji ya wanawake 29 kufikishwa mahakamani

14051 Pic+mahakamani TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Polisi wanaendelea kuchunguza watu 13 akiwamo kinara aliyekuwa anawabaka na kuwanyonga hadi kufa wanawake 29 katika matukio mbalimbali yaliyotokea maeneo ya Mwanza, Shinyanga na Geita.

Akizungumza leo Agosti 27, 2018 mkuu wa operesheni wa Polisi, Liberatus Sabasi amesema baada ya uchunguzi huo kukamilika mamlaka husika zitawafikisha mahakamani.

Sabasi amesema kwa sasa wanaendelea kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao ili kuwabaini wengine waliokuwa wanahusika na mauaji hayo.

“Tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika mamlaka husika zitawafikisha mahakamani watuhumiwa hao,” amesema Sabasi.

Juzi, Sabasi alitoa taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa kinara wa mauaji ya wanawake hao wilayani Misungwi na kwamba, baada ya kuhojiwa alikiri kutekeleza vitendo hivyo kwa kile alichodai ni kutokana na imani za kishirikina.

Amesema operesheni ya kuwakamata watuhumiwa hao wakiwamo waganga wa kienyeji ilianza Agosti  2017 katika maeneo ambayo mauaji hayo yalitokea.

Wanawake waliouawa ni Angelina Lumala (45) mkazi wa Kitongoji cha Ibelambasa kijiji cha Isakamawe; Ligwa Ngole (43) mkazi wa kitongoji cha Bujingwa; Kundi Laurent (35) na Mariamu Manila (30) wote wakazi wa Kitongoji cha Misasi juu A kijiji cha Misasi.

Hatahivyo, mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya nne za mkoa huo, aliagiza mamlaka zianze uchunguzi wa watu wanaohusika na mauaji hayo.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Misasi, Christina Ndakile alieleza kuwa kwa sasa hawaendi kufanya shughuli yoyote ya maendeleo wakihofia maisha yao.

Chanzo: mwananchi.co.tz