Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa mauaji ya mwanafunzi waanza kujitetea

42039 Mauaji+pic Watuhumiwa mauaji ya mwanafunzi waanza kujitetea

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Washitakiwa wawili katika kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta Sperius Eradius wameanza kujitetea baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kuwakuta na kesi ya kujibu.

Mshitakiwa wa kwanza mwalimu Respicius Mutazangira katika utetezi wake leo Ijumaa Februari 15, 2019 amekiri mwalimu wa nidhamu katika shule hiyo na marehemu alipelekwa kwake na mshitakiwa wa pili ambaye ni mwalimu Heriet Gerald.

Kesi hiyo namba 56/2018 inayosikilizwa na Jaji Lameck Mlacha, Mutazangira ameeleza alitoa adhabu kwa kuzingatia makubaliano ya kikao cha wazazi waliotaka watoto wenye tuhuma za wizi wachapwe viboko.

Ameieleza Mahakama anazo barua saba kutoka kwa walimu wakuu tofauti kumthibitisha kuwa mwalimu wa nidhamu na amekana kumuona mshitakiwa wa pili Heriet akitoa adhabu yoyote kwa marehemu.

Pia amekana kuifahamu miongozo na sheria zinazoweka utaratibu wa kutoa adhabu kwa mwanafunzi na kuwa alimkabidhi mwanafunzi huyo kwa mlezi wake akiwa mzima wa afya.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Hashimu Ngole umetaka mshitakiwa kuieleza mahakama kama mwalimu mkuu alipomteua kuwa mwalimu wa nidhamu alimkasimu madaraka ya kutoa adhabu.

Pia upande wa Jamhuri umemuuliza ni kitu gani kilitakiwa kuzingatiwa katika utoaji wa adhabu kati ya maazimio ya wazazi na miongozo ya kisheria ambapo mshitakiwa alisema miongozo ya kisheria inazingatiwa kwanza.

Kikao cha Mahakama Kuu kitaendelea baada ya mapumziko ambapo mshitakiwa wa pili Heriet Gerald anatarajiwa kujitetea.

Endelea kufuatilia Mwananchi



Chanzo: mwananchi.co.tz