Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa kumuua dereva wa bodaboda

Pingu Mkononi Edited Watuhumiwa kumuua dereva wa bodaboda

Sat, 17 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro, alisema watuhumiwa hao wanne wanadaiwa Julai 3, mwaka huu, walikula njama kwa kumtumia mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Malkia Luhende (42) kutekeleza mauaji hayo.

“Uchunguzi wetu umewezesha kupatikana kwa wahalifu hawa (bila kuyataja majina ya watatu) wakiwa na baadhi ya vielelezo muhimu, uchunguzi unaendelea,” alisema.

Pia alisema wamewakamata watu wawili wanaojihusisha na vitendo vya utapeli ambao ni Oswald Fidolini (47) maarufu kwa jina la Mbilo na Melkizedeck Mathayo (49) maarufu kama Hungo.

Alisema watuhumiwa hao wamekuwa wakijipatia fedha kutoka kwa wananchi kwa njia ya vitisho kwa kuwatishia na kutengeneza mazingira ya kuichafua serikali.

“Mara kadhaa wamekuwa wakijiita maofisa wa usalama wa taifa na makamisha wa polisi na maofisa wa TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa). Watu  hawa si watumishi wa serikali, tumewakamata,” alisema.

Kamanda Muliro alisema wamewapata watuhumiwa wengine zaidi ya 40 ambao wamekuwa wakijihusisha na unyang’anyi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba na kuiba, kupora kwa kutumia pikipiki maarufu kama vishandu.

Alisema katika matukio hayo wamekamata pikipiki tatu zinazotumiwa na wahalifu hao, runinga nane na kompyuta mpakato.

Kamanda huyo aliwaomba wananchi waendelee kutoa taarifa ili Dar es Salaam iendelee kuwa salama.

Chanzo: ippmedia.com