Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa kughushi kiwanja cha Malecela wapata dhamana

42033 Kiwanja+pic Watuhumiwa kughushi kiwanja cha Malecela wapata dhamana

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Washitakiwa watatu kati katika kesi ya kughushi kiwanja cha Waziri Mkuu wa zamani John Malecela, akiwemo diwani wa Makole (CCM) Abel Shauri wamepatiwa dhamana.

Dhamana ya washitakiwa hao imetolewa leo Ijumaa Februari 15,2019 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Dodoma, Godfrey Pius baada ya kushindikana juzi kutokana na pingamizi lililowekwa na upande wa Serikali.

Hakimu amewapa dhamana diwani Abel Shauri, Elias Stephen na Shaban Msovela baada ya kutimiza masharti huku msaidizi wa karibu wa Mzee Malecela Jackson Ndahani akirudishwa mahabusu katika Gereza Isanga baada ya kushindwa kutimiza masharti.

Juzi walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza wakiwa wamekaa kituo cha polisi kwa siku 16 na mawakili wa upande wa utetezi walijenga hoja za wateja wao kupatiwa dhamana lakini mahakama ikapanga kutoa uamuzi huo leo mchana.

Kwa pamoja watu hao wanashitakiwa kwa kosa la kughushi na kujipatia kiwanja namba 26 kitalu J katika eneo la Area D ambacho mmiliki wake ni John S. Malecela na kufanikiwa kukiuza kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Geodfrey Gao.

Kesi hiyo ambayo imevuta umati mkubwa wa watu imeahirishwa hadi Februari 28, 2019 huku upande wa mashitaka wakisema upelelezi haujakamilika



Chanzo: mwananchi.co.tz