Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa 45 mbaroni Mbeya, wapo wa mauaji

CBB2D1A1 F898 4F65 A76F 760EC77CE938.jpeg Watuhumiwa 45 mbaroni Mbeya, wapo wa mauaji

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: eatv.tv

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu  45 kwa tuhuma za makosa mbalimbali  ikiwemo watu 12 kuhusika na mauaji katika kipindi cha kuanzia Desemba mosi mpaka 23 mwaka huu

Kamishna Msaidizi wa Polisi,  mkoa wa Mbeya ACP Benjaman Kuzaga, amethibitisha hayo alipozungumza na wanahabari kuhusu mafanikio ya Jeshi hilo katika kipindi cha mwezi Desemba

Amesema kati ya watuhumiwa 12 wa mauaji tayari watano wamefikishwa mahakamani kwa ajali ya hatua za kisheria na wengine saba upelelezi unaendelea

Ameongeza kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na silaha aina ya Gobole ikiwa na risasi 50 pamoja na fataki 32 wilayani Chunya

“Haya ni miongoni mwa mafanikio ya Jeshi Polisi katika kipindi cha Desemba mosi mpaka 23 ambapo kupitia doria na misako mbalimbali tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 45 kwa makosa ya kupatikana na silaha bila kibali, dawa za kulevya, kuingiza bidhaa zilizopigwa marufuku, mauaji pamoja na nyara za Serikali,”amesema Kuzaga

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limeandaa utaratibu wa kupima kiwango cha ulevi  kwa madereva wote wa Mkoa huo, lengo ni kukabiliana na ajali za barabarani msimu  wa sikukuu za mwisho wa mwaka

Amesema tayari Polisi wametawanyika kwenye vizuizi mbalimbali mkoani Mbeya ili kupima watu na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.  

Chanzo: eatv.tv